08. Kinga ya nane ya janga la corona: Kutenda mazuri na kufanya wema

8- Kutenda mazuri na kufanya wema

Anas (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kufanya mazuri kunakinga kutokea kwa mambo mabaya, magonjwa na maangamivu. Wale wenye kufanya mazuri duniani ndio wenye kutaamiliwa vizuri Aakhirah.”

Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) amesema:

“Dawa bora kabisa ni kufanya matendo mema na mazuri, du´aa, swalah, kumnyenyekea Allaah na kutubia. Mambo haya yana taathira ya kuondosha magonjwa iliokubwa kuliko dawa za kimaumbile. Lakini ni kwa kiasi cha maandalizi, kukubali kwa nafsi, imani juu yake na manufaa yake.”[1]

[1] Zaad-ul-Ma´aad.

  • Mhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Ashru Waswaayaa lil-Wiqaayah min-al-Wabaa’, uk. 11-12
  • Imechapishwa: 05/04/2020