Swali 7: Unasemaje kuhusu makundi kwa hukumu ya jumla?

Jibu: Kila mwenye kwenda kinyume na Ahl-us-Sunnah ni mpotevu. Tuna kundi moja tu; nalo ni Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah[1]. Yule mwenye kwenda kinyume na kundi hili anaenda kinyume na mfumo wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Vilevile kila mwenye kwenda kinyume na Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ni katika Ahl-ul-Ahwaa´. Uhalifu huu unatofautiana inapokuja katika kusema kuwa mtu ni mpotevu au ni kafiri kwa kutegemea ukubwa wa uhalifu na kuwa mbali na haki.

[1] Nao ni pote lililonusuriwa na kundi lililookoka, Ahl-ul-Hadiyth, Ahl-ul-Athar na Salafiyyuun, kama walivoyasema hayo waziwazi jopo kubwa la wanazuoni waliotangulia na waliokuja baadaye. Mfano katika wao ni maimamu wanne na wanazuoni walio katika tabaka lao na wale waliokuja baada yao hata kama waliishi kipindi cha nyuma kabisa baada yao.

Si sahihi kuyaita mapote haya yanayoenda kinyume na kundi moja la waislamu “makundi”, kama ilivyosemwa mwanzoni na kubainishwa na Shaykh. Yaitwe “mapote” na “vyama”.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 28
  • Imechapishwa: 18/02/2017