07. Jambo la tatu linaloharibu swawm: yaliyo na maana ya kula na kunywa

3- Yanaungana na kula na kunywa yale mambo yaliyo na maana ya kula na kunywa. Haya yanafunguza. Mfano wa mambo hayo ni kama zile sindano za lishe. Kwa sababu mtu anaweza kutosheka nazo na asiwe na haja ya chakula. Jengine ni kuchota damu kunamfunguza yule mwenye kufunga. Kwa sababu damu ni ufupizo wa chakula na kinywaji. Lakini mara nyingi yule ambaye anahitajia sindano ya lishe au kuchotwa damu anakuwa ni mgonjwa ambaye anaruhusika kuacha kufunga.

Ama sindano zisizokuwa za lishe kwa mgonjwa hazimfunguzi mwenye kufunga. Ni mamoja sindano hizo zinadungwa kwenye misuli au kwenye mishipa. Kwa sababu sindano hizo sio kula wala kunywa wala hakuna maana ya kula na kunywa. Lakini lililo salama zaidi kwa mfungaji acheleweshe mpaka wakati wa usiku.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mukhtaswaru fiy Ahkaam-is-Swiyaam, uk. 14
  • Imechapishwa: 17/04/2019