c) Ni haramu kwa mwanamke wa Kiislamu kutia mwanya meno yake kwa ajili ya kutafuta urembo kwa chombo cha kupanulia ili atoe baina yake uwazi mdogo kwa ajili ya kutafuta uzuri.

Ama ikiwa meno yanaonekana vibaya na yanahitajia operesheni ya kuweka sawa kwa lengo la kuondesha muumbuko huu au meno yana maradhi ya kubadilisha rangi na akahitajia kuyafanya vizuri kwa lengo la kuondosha jambo hilo hakuna neno. Kwa sababu jambo hilo ni kwa lengo la matibabu na kuondosha muumbuko huu. Jambo hilo linafanyika kupitia daktari ambaye ni mtaalamu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tanbiyhaat, uk. 21-22
  • Imechapishwa: 22/10/2019