6- Yaziyd ametuhadithia, kutoka kwa Hammaad bin Salamah, kutoka kwa ´Ammaar bin Abiy ´Ammaar ambaye amesema:

“Ibn ´Abbaas alisoma Aayah ambapo myahudi aliyekuweko mbele yake akasema: “Laiti Aayah hii ingeliteremshwa kwetu basi tungeifanya siku hiyo kuwa ni sikukuu.” Ibn ´Abbaas akasema: “Hakika imeteremshwa siku ya idi, siku ya ijumaa na siku ya ´Arafah.”

7- Ismaa´iyl bin Ibraahiym ametuhadithia, kutoka kwa Daawuud bin Abiy Hind, kutoka kwa ash-Sha´biy aliyesema:

“Aliteremshiwa nayo (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na huku amesimama ´Arafah. Kipindi hicho shirki ilikuwa imesambaratishwa, nembo za kipidni cha kikafiri zimevunjwa na hakuna yeyote anayetufu kwenye Nyumba akiwa uchi.”[1]

Katika Aayah hii Allaah akataja namna ambavo ameikamilisha dini. Imesemekana kwamba ilishukwa nyusiku 81 kabla ya kufariki kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

8- Namnaa hiyo ndivo alituhadithia Hajjaaj, kutoka kwa Ibn Jurayj.

Lau imani ingekuwa imekamilishwa kwa kukiri ilihali Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiwa Makkah mwanzoni mwa utume wake, kama wanavosema watu hawa, basi ule ukamilishwaji unaozungumziwa usingekuwa na maana yoyote. Ni vipi kitu kimekamilika ikiwa wakati wote kinaongezwa mpaka mwisho wake?

[1] Cheni ya wapokezi ni Swahiyh pasi na Swahabah.

  • Mhusika: Imaam Abu ´Ubayd al-Qaasim bin Sallaam
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-Iymaan, uk. 26-27
  • Imechapishwa: 14/05/2021