07. Haya ndio malengo ya wenye kuwatukana Maswahabah

al-Jamaa´ah ni Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika al-Muhaajiruun na al-Answaar. Kwa sababu wao ndio walisuhubiana na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), wakapigana Jihaad bega kwa bega wakiwa pamoja naye, wakamnusuru, wakatusimulia dini na kutunukulia nayo. Wao ndio wakati kati kati yetu sisi na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hivyo wale ambao wanawatukana Maswahabah au kuwaponda malengo yao wanachotaka ni kuutokomeza Uislamu. Ni njama. Wao hawautaki Uislamu na hawakuona njama nyingine isipokuwa kuwatukana Maswahabah kwa kuwa wao ndio wakati kati walionukuu dini hii. Wakiwatukana Maswahabah kutakuwa kumebaki nini tena? Ni wepi walio kati na kati baina yetu sisi na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)? Haya ndio malengo ya wale wanaowatukana Maswahabah. Wanachotaka ni kukata mafungamano baina yetu na watu wa awali waliotangulia katika al-Muhaajiruun na al-Answaar. Malengo ni ili Ummah upotee. Vinginevyo ni lepi lililowafanya wao kuwatukana Maswahabah? Je, Maswahabah wamewaudhi kipi? Kati ya wao na Maswahabah kumeshapita karne nyingi tu. Kilichowapelekea wao kufanya hivi ni nyoyo zao zilizo na chuki. Maswahabah ndio waliobeba dini hii. Wanachotaka ni kukata mafungamano kati ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Ummah wake. Malengo yao ni kuiangusha dini hii.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Sharh-is-Sunnah, uk. 19
  • Imechapishwa: 01/10/2017