723- Amepokea vilevile ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Wanahudhuria swalah ya ijumaa watu watatu. Mtu wa kwanza anafanya upuuzi – hilo ni fungu lake. Mwingine anaihudhuria kwa du´aa. Huyu ni yule mtu anayemuomba Allaah; akitaka Atampa na akitaka atamnyima. Mtu wa tatu anaihudhuria kwa kukaa kimya na kunyamaza na asijipenyeze kwa muislamu yeyote na wala asimuudhi yeyote. Mtu huyo inafuta madhambi yake mpaka ijumaa nyingine na ukiongezea siku tatu. Kwa sababu Allaah amesema:

مَنْ جَاءَ بِالْحَسَنَةِ فَلَهُ عَشْرُ أَمْثَالِهَا

“Atakayekuja kwa tendo jema basi huyo atapata thawabu kumi mfano wake.”[1]

Ameipokea Abu Daawuud na Ibn Khuzaymah katika “as-Swahiyh” yake.

[1] 06:160

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/449)
  • Imechapishwa: 01/03/2019