07. Hadiyth “Qur-aan na swawm vitamuombea mja siku ya Qiyaamah… “


984- ´Abdullaah bin ´Amr (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Qur-aan na swawm vitamuombea[1] mja siku ya Qiyaamah. Funga itasema: “Ee Mola! Nilimzuia na chakula chake na matamanio yake; hivyo wacha nimuombee.” Qur-aan itasema: “Nilimzuia kulala usiku; hivyo wacha nimuombee.” Basi vimuombee.”[2]

Ameipokea Ahmad na at-Twabaraaniy katika “al-Kabiyr”. Ameipokea vilevile Ibn Abiyd-Dunyaa katika “Kitaab-ul-Juu´” kwa cheni ya wapokezi nzuri. Kadhalika al-Haakim amesema:

“Ni swahiyh juu ya masharti ya Muslim.”

[1] Vitamuombea kwa Allaah ili aingie Peponi. al-Munaawiy amesema:

“Maneno haya inawezekana ikawa kweli ambapo thawabu zikafanywa kiwiliwili na Allaah akaumba tamko ndani yake:

 وَاللَّـهُ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ

“Allaah juu ya kila jambo ni muweza.” (03:189)

Inawezekana vilevile ikawa ni mafumbbo na mifano.”

Hilo la kwanza ndio la sawa ambalo mtu anatakiwa kulitendea kazi na Hadiyth zote mfano wake ambapo matendo yatafanywa kiwiliwili na mfano wa hivo. Kuzipindisha maana Hadiyth mfano wa hizi sio katika mfumo wa Salaf (Radhiya Allaahu ´anhum). Bali ni katika mfumo wa Mu´tazilah na wale vifaranga vyao waliokuja nyuma. Hilo linapingana na sharti ya kwanza ya imani, nayo ni:

الَّذِينَ يُؤْمِنُونَ بِالْغَيْبِ

“Wale ambao huamini mambo yaliyofichikana.” (02:03)

Chunga usije kuwaiga usije kupotea na mla khasara.

[2] Nzuri na Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (01/579)
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy