07. Hadiyth “Mambo saba yanaendelea kulipwa kwa mja baada ya kufa kwake… “

73- Anas (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mambo saba yanaendelea kulipwa kwa mja baada ya kufa kwake ilihali amelala ndani ya kaburi lake: aliyefunza elimu, akachimba mfereji, akachimba kisima, akapanda mti wa mtende, akajenga msikiti, akaacha msahafu ambao ukarithiwa au akaacha mtoto ambaye akamuombea msamaha baada ya kufa kwake.”[1]

Ameipokea al-Bazzaar na Abu Nu´aym katika “al-Hilyah” ambaye amesema:

“Hadiyth hii ni geni kutoka kwa Abu Qataadah. Abu Nu´aym amepwekeka nayo katika kuipokea kutoka kwa al-´Arzamiy.”

[1] Nzuri kupitia zengine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/140)
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy