07. Hadiyth “Allaah anapenda zitendewe kazi ruhusa Zake… “

1059- Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) anapenda zitendewe kazi ruhusa Zake kama ambavo anachukia kuasiwa.”[1]

 Ameipokea Ahmad kwa cheni ya wapokezi Swahiyh, al-Bazzaar, at-Twabaraaniy katika “al-Awsatw” kwa cheni ya wapokezi nzuri, Ibn Khuzaymah na Ibn Hibbaan katika “as-Swahiyh” zao. Katika upokezi wa Ibn Khuzaymah imekuja:

“Allaah anapenda zitendewe kazi ruhusa Zake kama anavopenda asiasiwe.”[2]

[1] Nzuri na Swahiyh.

[2] Nzuri na Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/617)
  • Imechapishwa: 22/04/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy