07. Dalili ya sita kutoka katika Sunnah juu ya mikono ya Allaah

6- Abu Hurayrah amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mkono wa kuume wa Allaah (´Azza wa Jall) umejaa. Haupungui kitu kwa kutoa mchana na usiku. Kwenye mkono Wake mwengine kuna mizani ambayo anapandisha na anashusha.”[1]

Ameipokea al-Bukhaariu na Muslim.

[1] al-Bukhaariy (4684), Muslim (993), Ahmad (2/242) na at-Tirmidhiy (3045) aliyesema:

“Hadiyth hii ni nzuri na Swahiyh na inafasiri Aayah isemayo:

وَقَالَتِ الْيَهُودُ يَدُ اللَّـهِ مَغْلُولَةٌ ۚ غُلَّتْ أَيْدِيهِمْ وَلُعِنُوا بِمَا قَالُوا ۘ بَلْ يَدَاهُ مَبْسُوطَتَانِ يُنفِقُ كَيْفَ يَشَاءُ

“Mayahudi wakasema: “Mkono wa Allaah imefumbwa”. Mikono yao ndio iliyofumbwa na wamelaaniwa kwa yale waliyoyasema. Bali mikono Yake imekunjuliwa hutoa atakavyo.” (05:64)

Hadiyth imepokelewa na maimamu. Tunaiamini kama ilivyokuja pasi na kuipindisha wala kuifanyia namna. Hivo ndivo walivosema maimamu akiwemo Sufyaan ath-Thawriy, Maalik bin Anas, Ibn ´Uyaynah na Ibn-ul-Mubaarak; zinatakiwia kusimiliwa na kuziamin pasi na kuzifanyia namna.”

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ithbaat-ul-Yad li-Laah Swifatan min Swifwaatih, uk. 18
  • Imechapishwa: 17/06/2019