07. Dalili juu ya mguu wa Allaah 7

7- Abu Salamah ametuhadithia: Hammaad ametuhadithia, kutoka kwa ´Atwaa´ bin as-Saa-ib, kutoka kwa ´Ubaydullaah bin ´Abdillaah bin ´Utbah, kutoka kwa Abu Sa´iyd ambaye ameeleza ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kasema:

“Pepo na Moto vilizozana ambapo Moto ukasema: “Ndani yangu wanaingia wakandamizaji, wafalme na watukufu.” Pepo nayo ikasema: “Ndani yangu wanaingia watu mafukara na masikini.” Ndipo Akasema kuuambia Moto: “Wewe ni adhabu Yangu ambayo namsibu yule Ninayemtaka.” Akasema kuiambia Pepo: “Wewe ni huruma Yangu inayokienea kila kitu. Kila mmoja wenu atajazwa.” Kuhusu Moto kutatupwa ndani yake na utasema:

هَلْ مِن مَّزِيدٍ

“Hakuna zaidi?”[1]

mara tatu mpaka pale (Tabaarak wa Ta´ala) Atapoweka unyayo Wake juu yake. Hapo ndipo utajikusanya na kusema: “Tosha, tosha.”

Katika upokezi wa Abu Hurayrah imekuja ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema:

“Tosha, tosha.”

[1] 50:30

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin ´Umar ad-Daaraqutwniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-us-Swifaat, uk. 42-43
  • Imechapishwa: 21/10/2017