07. ash-Shawkaaniy kuhusu sherehe ya usiku wa nusu ya Sha´baan


´Allaamah ash-Shawkaaniy (Rahimahu Allaah) amesema katika “al-Fawaaid al-Majmu´ah” yafuatayo:

“Hadiyth isemayo: “Ee ´Aliy! Yeyote atakayeswali Rak´ah mia moja katika usiku wa nusu ya Sha´baan ambapo akasoma katika kila Rak´ah ufunguzi wa Kitabu, “Sema: “Allaah ni Mmoja” mara kumi, isipokuwa Allaah atamkidhia kila haja… “[1]

Ibn Hibbaan amepokea kupitia kwa ´Aliy:

“Inapokuwa usiku wa nusu ya Sha´baan, basi simameni usiku wake na fungeni mchana wake.”

Ni dhaifu.

Amesema tena katika “al-La-aalaiy”:

“Rak´ah mia moja katika usiku wa nusu ya Sha´baan hali ya kumtakasia nia Allaah zikiambatana na urefu wa fadhilah zake” ambayo imepokelewa na ad-Daylamiy na wengineo imetungwa. Wapokezi wake wote kupitia njia zake tatu hawatambuliki na ni wanyonge. Akasema: “Rak´ah kumi na mbili hali ya kumtakasia nia Allaah mara thelathini na Rak´ah kumi na nne” imetungwa.

Wako wanazuoni kadhaa waliodanganyika na Hadiyth hizi. Kama mtunzi wa “al-Ihyaa´” na wengineo. Kama ambavo wako wanazuoni kadhaa wanaofasiri Qur-aan waliodanganyika nazo. Nimepokea swalah kuhusu usiku huu – nikikusudia usiku wa nusu ya Sha´baan – kwa njia mbalimbali ambazo zote ni batili na zimetungwa. Haya hayapingani na upokezi wa at-Tirmidhiy kupitia kwa ´Aaishah kuhusu kwenda kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) al-Baqiy´, kushuka kwa Mola usiku wa nusu ya Sha´baan katika mbingu ya chini na kwamba akasamehe zaidi ya wingi wa nywele za Kalb cha kondoo. Tunachozungumzia ni kuhusu swalah iliyotungwa katika usiku huu. Licha ya kwamba Hadiyth ya ´Aaishah hii iko na unyonge na kukatika kwa cheni ya wapokezi. Vilevile Hadiyth ya ´Aliy, ambayo tumetangulia kuitaja kuhusu kusimama usiku wake, haipingani kitendo cha swalah hii kuwa imetungwa. Ukiongezea kama tulivosema ya kwamba iko na unyonge.”

[1] Imetungwa. Katika matamshi yake kumesemwa wazi zile thawabu anazopata yule mwenye kufanya hivo, jambo ambalo hapati shaka yoyote yule mwenye uwezo wa kupambanua juu ya kutungwa kwake. Wapokezi wake hawamtambuliki. Imepokelewa kutoka katika njia ya pili na ya tatu ambazo zote zimetungwa na aidha wapokezi wake hawatambuliki. Vilevile amesema katika “al-Mukhtaswar”:

“Hadiyth kuhusu kuswali usiku wa nusu ya Sha´baan ni batili.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tahdhiyr minal-Bid´ah, uk. 27-29
  • Imechapishwa: 18/01/2022