07. Anachotakiwa kufanya mwenye kuota

39- Abu Salamah bin ´Abdir-Rahmaan ameeleza kwamba amemsikia Abu Qataadah bin Rab´iy akisema kwamba amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

Ndoto njema inatoka kwa Allaah na ndoto mbaya inatoka kwa Shaytwaan. Mmoja wenu akiona ndoto mbaya apulize kushotoni kwake mara tatu wakati atapoamka na amuombe Allaah kinga kutokana na shari yake. Haitomdhuru Allaah Akipenda.”

Abu Salamah amesema:

“Nilikuwa naona ndoto ambazo ni nzito kwangu kuliko jibali. Baada ya kusikia Hadiyth hii sikuwa nazijali.”

Katika upokezi mwingine amesema:

“Nilikuwa naona ndoto ambazo zinanitia wasiwasi mpaka nilipomsikia Abu Qataadah akisema: “Nilikuwa nikiona ndoto ambazo zinanifanya kuwa mgonjwa mpaka nilipomsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

Ndoto njema inatoka kwa Allaah na ndoto mbaya inatoka kwa Shaytwaan. Mmoja wenu akiona ndoto mbaya apulize kushotoni kwake mara tatu wakati atapoamka na amuombe Allaah kinga kutokana na shari yake. Haitomdhuru Allaah Akipenda.”

40- Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mmoja wenu akiona ndoto mbaya basi na apulize kushotoni kwake mara tatu, amuombe Allaah kinga kutokana na Shaytwaan mara tatu na abadili upande aliokuwa amelalia.”

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 41-42
  • Imechapishwa: 21/03/2017