07. al-Albaaniy kuhusu jamii ya Hanaabilah hii leo

Jambo la tano ni kwamba al-Albaaniy (Rahimahu Allaah) amemzingatia Ibn Taymiyyah, Ibn-ul-Qayyim, Hanaabilah wote na wafuasi wote wa Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab katika kundi la wale wenye kuamini Allaah (´Azza wa Jall) kuwepo juu ya viumbe na kuamini lile swali la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Allaah yuko wapi?” Akajibu: “Juu ya mbingu.” Akamuuliza: “Mimi ni nani?” Akajibu: “Wewe ni Mtume wa Allaah.” Akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Mwache huru. Kwani hakika ni muumini.”[1]

Amewavua kutoka katika jamii ya kipindi cha kikafiri na akabainisha kwamba wamepatia.

[1] Muslim (537).

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fath ar-Rabbaaniy fiyd-Difaa´ ´an-ish-Shaykh Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy, uk. 28
  • Imechapishwa: 27/10/2018