06. Virusi vya corona – Janga kubwa ni mtihani katika dini

6- Hakika janga kubwa ni msiba katika dini; kwani ndio msiba mkubwa duniani na Aakhirah. Msiba wa dini ndio mwisho wa khasara. Pindi yule muislamu aliyepewa mtihani anapokumbuka jambo hilo basi anamshukuru Allaah kwa usalama wa dini yake. al-Qaadhwiy Shurayh (Rahimahu Allaah) amesema:

“Pindi ninapojaribiwa kwa msiba basi humshukuru Allaah mara nne: Namshukuru Allaah kutokana na kwamba haukuwa mkubwa zaidi kuliko ulivo hivi sasa, namshukuru kwa vile amenijaalia kuweza kuuvumilia, namshukuru kwa kuniwafikisha kuweza kusema “Hakika sisi ni wa Allaah na hakika Kwake ndiko tutarejea” hali ya kutarajia malipo na namshukuru kwamba hakuufanya ukaisibu dini yangu.”[1]

Namuomba Allaah atulinde sote kwa hifdhi Yake na atutunuku usalama katika dini na dunia yetu, familia zetu na mali zetu.

[1] al-Bayhaqiy katika ”Shu´b-ul-Iymaan”.

  • Mhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://ar.islamway.net/article/80439/%D9%81%D9%8A%D8%B1%D9%88%D8%B3-%D9%83%D9%88%D8%B1%D9%88%D9%86%D8%A7-%D8%A7%D9%84%D8%AC%D8%AF%D9%8A%D8%AF-%D9%81%D9%8A%D8%B1%D9%88%D8%B3-%D8%A7%D9%84%D8%B5%D9%8A%D9%86
  • Imechapishwa: 12/03/2020