06 – Uchumi

Qur-aan imebainisha misingi ya kiuchumi ambayo tanzu zote zinarejea kwayo, mambo ya kiuchumi yarejea katika misingi miwili:

1 – Njia nzuri ya kuchuma pesa.

2 – Njia ya kuzitumia.

Tazama jinsi Kitabu cha Allaah kinavyombainishia mwanadamu namna anavyotakiwa kuchuma pesa kwa njia inayolingana na marua na dini. Amesema:

فَإِذَا قُضِيَتِ الصَّلَاةُ فَانتَشِرُوا فِي الْأَرْضِ وَابْتَغُوا مِن فَضْلِ اللَّـهِ

“Na inapomalizika swalah, basi tawanyikeni katika ardhi na tafuteni fadhilah za Allaah.”[1]

وَآخَرُونَ يَضْرِبُونَ فِي الْأَرْضِ يَبْتَغُونَ مِن فَضْلِ اللَّـهِ

“Na wengine wanasafiri katika ardhi wanatafuta fadhilah za Allaah.”[2]

لَيْسَ عَلَيْكُمْ جُنَاحٌ أَن تَبْتَغُوا فَضْلًا مِّن رَّبِّكُمْ

“Hapana kwenu dhambi kutafuta fadhilah toka kwa Mola wenu.”[3]

إِلَّا أَن تَكُونَ تِجَارَةً عَن تَرَاضٍ مِّنكُمْ

“… isipokuwa iwe biashara kwa kuridhiana kati yenu.”[4]

وَأَحَلَّ اللَّـهُ الْبَيْعَ

“Allaah amehalalisha biashara.”[5]

فَكُلُوا مِمَّا غَنِمْتُمْ حَلَالًا طَيِّبًا

“Kuleni katika mlivyopata ngawira [hivyo ni] halali vizuri.”[6]

Tazama namna inavyoamrisha utumiaji wa uchumi:

وَلَا تَجْعَلْ يَدَكَ مَغْلُولَةً إِلَىٰ عُنُقِكَ وَلَا تَبْسُطْهَا كُلَّ الْبَسْطِ

“Na wala usifanye mkono wako kama uliofungwa shingoni mwako [kama bakhili] na wala usiukunjue wote kabisa [ukatoa kwa fujo].”[7]

وَالَّذِينَ إِذَا أَنفَقُوا لَمْ يُسْرِفُوا وَلَمْ يَقْتُرُوا وَكَانَ بَيْنَ ذَٰلِكَ قَوَامًا

“Na wale ambao wanapotoa huwa hawafanyi israfu na wala hawafanyi uchoyo na wanakuwa wastani baina ya hayo.”[8]

وَيَسْأَلُونَكَ مَاذَا يُنفِقُونَ قُلِ الْعَفْوَ

“Na wanakuuliza nini watoe. Sema: “Yaliyokuzidieni.””[9]

Tazama namna inavyokataza utumiaji wa haramu:

إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا يُنفِقُونَ أَمْوَالَهُمْ لِيَصُدُّوا عَن سَبِيلِ اللَّـهِ ۚفَسَيُنفِقُونَهَا ثُمَّ تَكُونُ عَلَيْهِمْ حَسْرَةً ثُمَّ يُغْلَبُونَ ۗ وَالَّذِينَ كَفَرُوا إِلَىٰ جَهَنَّمَ يُحْشَرُونَ

“Hakika wale waliokufuru wanatoa mali zao ili wawazuie [watu] kutokamana na njia ya Allaah. Basi watazitoa, kisha itakuwa ni majuto juu yao, kisha watashindwa. Na wale waliokufuru watakusanywa kwenye Moto.”[10]

[1] 62:10

[2] 73:20

[3] 02:198

[4] 04:29

[5] 02:275

[6] 08:69

[7] 17:29

[8] 25:67

[9] 02:219

[10] 08:36

  • Mhusika: Imaam Muhammad Amiyn ash-Shanqiytwiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Islaam diyn al-Kaamil, uk. 18-19
  • Imechapishwa: 13/06/2023