06. Shaam ndiko wataishi watu wema katika zama za mwisho

Kumeshatajwa katika Hadiyth:

”Shikamana na Shaam kwani hakika ndio ardhi bora ya Allaah.” Huko Allaah huwateua waja Wake bora. Iwapo mtakataa basi chagueni Yemen na kunyweni kutoka chemchem yake. Hakika Allaah amechukua jukumu juu yangu la kuiangalia Shaam na watu wake.”

35- Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kutakuwa kuhajiri baada ya kuhajiri. Wabora wa ardhini watakuwa wale waliohajiri sehemu aliyohajiri Ibraahiym. Katika ardhi kutabaki wale watu waovu. Ardhi yao itawachukia na nafsi ya Mwingi wa huruma itawachukia. Moto utawakusanya pamoja na ndegere na nguruwe.”

al-Haakim amesema:

“Ni Swahiyh kwa masharti ya al-Bukhaariy na Muslim.”

Hata hivyo aliyoyasema yanatakiwa kuangaliwa vizuri[1].

36- Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Watapoangamia watu wa Shaam basi kutakuwa hakuna kheri kwenu. Hakutoacha kuwepo kikundi katika Ummah wangu chenye kunusuriwa. Hakitodhurika na wale wenye kuwakosesha nusura mpaka isimame Saa.”

Ameipokea Imaam Ahmad na at-Tirmidhiy aliyesema:

“Hadiyth ni Swahiyh.”

37- Ibn Mas´uud amesema:

“Tisa ya kumi ya wema iko Shaam na iliobaki iko katika miji mingine. Tisa ya kumi ya uovu iko katika miji mingine na moja ya kumi iko Shaam. Mtafikiwa na wakati ambapo mali inayopendwa zaidi ya mtu ni punda zinazombeba kumpeleka Shaam.”

38- Ka´b-ul-Ahbaar amesema:

“Wema umegawanyika sehemu kumi. Tisa iko Shaam na iliyobaki iko ardhini kwengine.”

39- al-Waliyd bin Swaalih amesema:

“Katika kile kitabu cha kwanza Allaah anasema kuiambia Shaam: “Wewe ni wa kipekee. Kutokea kwako ndiko kuna kufufuliwa na kwako ndiko kuna mkusanyiko. Ndani yako kuna moto Wangu na nuru Yangu. Yule anayekuja kwako kwa furaha anapata huruma Wangu na yule anayetoka kwako kwa kutokukupenda anapata hasira Zangu. Una nafasi ya watu wake kama ambavyo kifuko cha uzazi cha mama kina nafasi ya mtoto wake.”

40- Imepokelewa kupitia njia nyingi namna Ka´b-ul-Ahbaar alivyopata katika vile vitabu vilivyotangulia imeandikwa:

“Hakika mimi nimesoma katika Kitabu cha Allaah Tawraat ya kwamba Shaam ndio hazina ya Allaah katika ardhi na huko ndio kuna hazina ya Allaah kwa waja Wake.”

41- Wahb bin Munabbih amesema:

“Nimesoma kuhusu Shaam mara nyingi katika vitabu vilivyotangulia mpaka mtu anaweza kudhania kuwa Shaam haiko isipokuwa tu kwa ajili ya Allaah.”

42- al-Hasan al-Baswriy amesema:

“Wabora wa Shaam ni wabora kwenu. Waovu wa Shaam ni bora kuliko waovu wenu.” Wakasema: “Ee Abu Sa´iyd! Ni kipi kinachokufanya kusema hivo?” Akasema: “Kwa kuwa Allaah (Ta´ala) anasema:

وَنَجَّيْنَاهُ وَلُوطًا إِلَى الْأَرْضِ الَّتِي بَارَكْنَا فِيهَا لِلْعَالَمِينَ

“Tukamuokoa na Luutw kuelekea ardhi ambayo tumeibariki kwa ajili ya walimwengu.”[2]

43- Ismaa´iyl bin ´Ayyaash amesema:

“Wakati nilipotoka kwa al-Mahdiy nilikutana na Hushaym bin Bashiyr ambaye alinambia: “Ee Abu ´Utbah! Tumewasikia waalimu zetu wakisema: “Wema wenu ni bora kuliko wabora wetu na watenda madhambi wenu ni bora kuliko watenda madhambi wetu.”

44- Ya´quub bin Shaybah amepokea kwa mlolongo wa wapokezi wake kupitia kwa al-Haarith bin ´Umayrah aliyesimulia ya kwamba alifika kwa Ibn Mas´uud ambaye alimwambia:

“Mtoto wa ndugu yangu! Wewe unatokea wapi?” al-Haarith akasema: “Shaam.” Ndipo akasema: “Ni maoneo mazuri yaliyoje Shaam lau tu wasingelijishuhudia wao wenyewe ya kwamba ni katika watu wa Peponi.”

[1] Ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”as-Swahiyhah” (3203).

[2] 21:71

  • Mhusika: Imaam ´Abdur-Rahmaan bin Rajab al-Baghdaadiy al-Hanbaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwaa-il-ush-Shaam, uk. 47-58
  • Imechapishwa: 09/02/2017