06. Nguzo tano za imani kwa watoto

وأصول الإيمان ستة

Nguzo za imani ni sita. Ni kuamini:

أن تؤمن بالله، وملائكته، وكتبه، ورسله، واليوم الآخر، وبالقدر خيره وشره

1- Allaah.

2- Malaika Wake.

3- Vitabu Vyake.

4- Mitume Wake.

5- Siku ya mwisho.

6- Mazuri na mabaya ya Qadar.

ودليله ما في (الصحيح) من حديث عمر بن الخطاب

Dalili ya hilo ni Hadiyth Swahiyh iliyosimuliwa na ´Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´anh):

بينما نحن جلوس عند رسول الله – صلى الله عليه وسلم – ذات يوم إذ طلع علينا رجل شديد بياض الثياب، شديد سواد الشعر، لا يرى عليه أثر السفر، ولا يعرفه منا أحد، حتى جلس إلى النبي صلى الله عليه وسلم، فأسند ركبتيه إلى ركبتيه، ووضع كفيه على فخذيه، وقال: يا محمّد أخبرني عن الإسلام؟! فقال رسول الله صلى الله عليه وسلم: “الإسلام أن تشهد أن لا إله إلا الله، وأن محمداً رسول الله، وتقيم الصلاة، وتؤتي الزكاة، وتصوم رمضان، وتحج البيت إن استطعت إليه سبيلاً”، قال: صدقت. فعجبنا له يسأله ويصدّقه، قال: فأخبرني عن الإيمان؟ قال: “أن تؤمن بالله وملائكته وكتبه ورسله واليوم الآخر وتؤمن بالقدر خيره وشره”، قال: صدقت. قال: فأخبرني عن الإحسان؟ قال: “أن تعبد الله كأنك تراه فإن لم تكن تراه فإنه يراك”. قال: فأخبرني عن الساعة؟ قال: “ما المسؤول عنها بأعلم من السائل”، قال: فأخبرني عن أماراتها؟ قال: “أن تلد الأمة ربتها، وأن ترى الحفاة العراة العالة رعاء الشاء يتطاولون في البنيان”، ثم انطلق. فلبثت ملياً، ثم قال: “يا عمر أتدري من السائل؟” قلت: الله ورسوله أعلم، قال:  فإنه جبريل أتاكم يعلّمكم دينكم

“Siku moja tulipokuwa tumekaa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alitutokea mtu ambaye nguo zake zilikuwa nyeupe pepe na nywele zake zilikuwa nyeusi sana. Hakuwa na alama ya kuonesha kuwa ni msafiri na wala hapakuwa na hata mmoja katika sisi aliyemtambua. Alienda akakaa karibu na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akaweka magoti yake karibu na mago yake na akaweka viganja vyake juu ya mapaja yake.” Akasema: “Ee Muhammad, nieleze kuhusu Uislamu!” Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasema: “Uislamu ni kushuhudia kuwa hapana mola anayeabudiwa kwa haki isipokuwa Allaah na Muhammad ni Mtume wa Allaah, kusimamisha Swalah, kutoa Zakaah, kufunga Ramadhaan na kwenda kuhiji ukiweza.” Akasema: “Umesema kweli.” Tukashangazwa kwa kumuuliza kwake Mtume na kumsadikisha. Kisha akasema: “Nieleze kuhusu imani!” Akasema: “Ni kumuamini Allaah, Malaika Wake, Vitabu Vyake, Mitume Wake na siku ya Mwisho na kuamini Qadar; kheri na shari yake.” Akasema: “Umesema kweli!” Akasema: “Nielezee kuhusu Ihsaan!” Akasema: “Ni kumuabudu Allaah kama vile unamuona. Ikiwa wewe humuoni, basi Yeye Anakuona.” Akasema: “Nieleze kuhusu Qiyaamah.” Akasema: “Muulizwaji si mjuzi kama asivyo vilevile muulizaji.” Akasema: “Nieleze kuhusu alama zake!” Akasema: “Kijakazi kumzaa bibi yake na utaona wachunga wanaenda miguu chini, uchi na mafukara wakishindana kujenga majumba marefu.” Amesema: “Kisha akaondoka na tukatulia muda mrefu. Halafu akasema (Swallla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Ee ‘Umar! Je, unamjua ni nani yule aliyekuwa akiuliza?” Nikajibu: “Allaah na Mtume Wake ndio wanajua zaidi.” Akasema Mtume: “Ilikuwa ni Jibriyl ambaye amekuja kuwafundisha Dini yenu.””

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ta´liym-us-Swibyaan at-Tawhiyd, uk. 18-21
  • Imechapishwa: 25/03/2017