1- Muhammad bin ´Aliy bin Husayn amesema:

“Pindi mtu anapofikisha miaka 40 hunadi mwenye kunadi mbinguni: “Safari inakaribia. Andaa chakula chako.”

2- Mwenye busara anatakiwa kuwa mwangalifu kutoufanya moyo wake kuwa mgumu. Mfalme akiwa mzuri basi na askari pia huwa wazuri na mfalme akiharibika basi na askari pia huharibika.

3- ´Umar bin al-Khattwaab amesema:

“Keti na wale wenye kutubia. Mioyo yao ni laini.”

4- Kuna mtu alimwambia al-Hasan al-Baswriy:

“Mambo yako vipi? Vipi hali yako?” Akajibu:

“Ni vipi itakuwa hali ya ambaye anakutana na asubuhi na jioni hali ya kusubiri mauti yamjie na wala hajui ni kipi kitachopitika?”

5- al-Hasan al-Baswriy:

“Kitendo bora ni uchaji Allaah na mazingatio.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Hibbaan al-Bustiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Rawdhat-ul-´Uqalaa’ wa Nuzhat-ul-Fudhwalaa’, uk. 31-32
  • Imechapishwa: 12/11/2016