Kuwaamini Malaika maana yake ni kusadikisha uwepo wao na kwamba wao ni viumbe miongoni mwa viumbe wa Allaah. Allaah kawaumba kutokamana na nuru. Allaah amewaumba ili wamuabudu na watekeleze maamrisho Yake ulimwenguni. Amesema (Ta´ala):

بَلْ عِبَادٌ مُّكْرَمُونَ لَا يَسْبِقُونَهُ بِالْقَوْلِ وَهُم بِأَمْرِهِ يَعْمَلُونَ

“Bali ni waja waliokirimiwa. Hawamtangulii kwa kauli nao kwa amri Yake wanafanya.”[1]

جَاعِلِ الْمَلَائِكَةِ رُسُلًا أُولِي أَجْنِحَةٍ مَّثْنَىٰ وَثُلَاثَ وَرُبَاعَ ۚيَزِيدُ فِي الْخَلْقِ مَا يَشَاءُ

“Mwenye kuwafanya Malaika kuwa wajumbe wenye mbawa mbilimbili na tatutatu na nnenne. Huzidisha katika uumbaji atakavyo.”[2]

[1] 21:26-27

[2] 35:01

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Min Usuwl ´Aqiydah Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah, uk. 18-19
  • Imechapishwa: 12/05/2022