06. Msingi ambao al-Jamaa´ah imejengwa juu yake

Imaam al-Barbahaariy (Rahimahu Allaah) amesema:

3- Msingi ambao al-Jamaa´ah imejengwa juu yake ni Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na ni Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Yule asiyechukua kutoka kwao amepotea na kuzusha. Kila Bid´ah ni upotevu na upotevu na watu wake ni Motoni.

al-Jamaa´ah ni Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na waliokua baada yao katika Taabi´uun, waliokuja baada ya Taabi´uun na karne bora. Hawa ndio al-Jamaa´ah na waliokuja nyuma wanaofuata mwongozo wao. Hawa ndio al-Jamaa´ah ambao ni lazima kwa Waislamu kuwa pamoja nao. Hata akifikwa na yakufikwa katika maudhi, matishio na changamoto mbalimbali, awe na uvumilivu katika haya midhali yuko katika haki. Asikengeuke na haki. Kinyume chake anatakiwa awe na subira juu ya yale yatayomfika. Vinginevyo atakuwa mateka ya wapindaji, walinganizi wapotevu na walinganizi waovu. Amesema (Ta´ala):

وَالسَّابِقُونَ الْأَوَّلُونَ مِنَ الْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنصَارِ وَالَّذِينَ اتَّبَعُوهُم بِإِحْسَانٍ رَّضِيَ اللَّـهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ

“Wale waliotangulia awali miongoni mwa al-Muhaajiriyn na al-Answaar na wale waliowafuata kwa wema Allaah ameridhika nao nao wameridhika Naye.” (09:100)

Baada ya (Ta´ala) kutaja al-Muhaajiruun na al-Answaar katika Suurah “al-Hashr” akasema:

َالَّذِينَ جَاءُوا مِن بَعْدِهِمْ يَقُولُونَ رَبَّنَا اغْفِرْ لَنَا وَلِإِخْوَانِنَا الَّذِينَ سَبَقُونَا بِالْإِيمَانِ وَلَا تَجْعَلْ فِي قُلُوبِنَا غِلًّا لِّلَّذِينَ آمَنُوا رَبَّنَا إِنَّكَ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ

“Na wale waliokuja baada yao ni wenye kusema: “Mola wetu!Tusamehe sisi na ndugu zetu ambao wametutangulia kwa imani na wala Usijaalie katika nyoyo zetu mafundo kwa wale walioamini – Mola wetu! Hakika ni Mwenye huruma mno, Mwenye kurehemu.” (59:10)

Waliokuja nyuma wawaige watu wa haki na wema waliotangulia. Hata kama baina yao kutakuwa kumeshapita muda mrefu. Linalomlazimu ni kulazimiana na yale waliyokuwemo pasi na kujali uzito ataoupata. Awe na subira.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Sharh-is-Sunnah, uk. 18-19
  • Imechapishwa: 01/10/2017