10. ´Aqiydah ya Ahl-us-Sunnah juu ya ambaye haswali

Hakuna kitendo chochote kukiacha ni kufuru isipokuwa swalah peke yake. Yule mwenye kuiacha kabisa basi amekufuru. Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wameafikiana juu ya hilo. ´Abdullaah bin Shaqiyq amesema:

“Hakuna kitu Maswahabah wa Mtume wa Allaah ambacho walikuwa wakionelea kukiacha kwake ni kufuru isipokuwa swalah.”

Ameipokea at-Tirmidhiy.

Takfiyr ni haki ya Allaah. Asiwepo atayemkufurisha yeyote isipokuwa tu yule ambaye amekufurishwa na Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) au mtu ambaye waislamu wameafikiana juu ya kumkufurisha.

Ambaye atamkufurisha mtu kwa kitu kisichokuwa ukafiri ambacho kimesimama juu ya hoja zilizo wazi kutoka katika Qur-aan tukufu, Sunnah Swahiyh au maafikiano, basi mtu huyo anastahiki adhabu kali na kuaziriwa. Kwa sababu al-Bukhaariy amepokea kupitia kwa Thaabit bin adh-Dhwahhaak (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kumtuhumu muumini ukafiri basi ni kama kumuua.”

Kufuru inaweza kupatikana kwa kutamka neno, kufanya kitendo na kuitakidi imani fulani ya kufuru ambayo hakuna tofauti yoyote inayozingatiwa. Sio miongoni mwa sharti za kufuru mtu aonelee kuwa ni halali.

Kuna tofauti kati ya kukufurisha kwa jumla na kumkufurisha mtu maalum. kukufurisha kwa jumla ni kama makemeo na matishio ya jumla. Mtu anatakiwa kusema vile ilivyo kama ambavyo haikufungamana na kwa ujumla wake. Mfano wa hilo ni kama walivyosema maimamu:

“Mwenye kusema Qur-aan imeumbwa ni kafiri.”

Ibn Khuzaymah (Rahimahu Allaah) amesema:

“Ambaye hathibitishi kuwa Allaah amelingana juu ya ´Arshi na yuko juu ya mbingu ya saba ni kafiri ambaye damu yake ni halali. Mali yake inakuwa fai.”

Kuhusu kumkufurisha mtu maalum ni lazima masharti yatimie na kusiwepo vikwazo. Kukufurisha kwa jumla ambako hakufungamana hakupelekei kumkufurisha mtu maalum mpaka yatimie masharti ya kukufurisha na vikwazo viondoke.

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas
  • Marejeo: al-Mu´taqad as-Swahiyh, uk. 70
  • Imechapishwa: 21/06/2020