06. Mfano wa kwanza kuonyesha jinsi Raafidhwah wanavodai kuwa Maswahabah wamepotosha Qur-aan

al-Qumiy (01/100) amesema:

“Kauli Yake:

إِنَّ اللَّـهَ اصْطَفَىٰ آدَمَ وَنُوحًا وَآلَ إِبْرَاهِيمَ وَآلَ عِمْرَانَ عَلَى الْعَالَمِينَ

“Hakika Allaah Amemteua Aadam na Nuuh na kizazi cha Ibraahiym na kizazi cha ‘Imraan juu ya walimwengu.” (03:33)

Aayah iko kwa jumla lakini maana yake ni maalum pale ambapo Amewateua tu katika wakati ule waliokuwa wakieshi. Mwanachuoni (´alayhis-Salaam) amesema: “Aayah iliteremshwa ikiwa hivi:

“… na kizazi cha ´Imraan na kizazi cha Muhammad juu ya walimwengu.”

lakini wakawa wameondosha “kizazi cha Muhammad” kwenye Kitabu.”

al-´Ayyaashiy (01/168) amesema:

“Hishaam bin Saalim ameeleza kuwa alimuuliza Abu ´Abdillaah kuhusiana na Kauli ya Allaah:

إِنَّ اللَّـهَ اصْطَفَىٰ آدَمَ وَنُوحًا

“Hakika Allaah Amemteua Aadam na Nuuh…”

Akasema: “Inatakiwa iwe kizazi cha Ibraahiym na kizazi cha Muhammad, lakini wakabadili jina.”

al-´Ayyaashiy (01/169) amesema:

“Ayyuub amesema: “Abu ´Abdillaah alinisikia nikisoma:

إِنَّ اللَّـهَ اصْطَفَىٰ آدَمَ وَنُوحًا وَآلَ إِبْرَاهِيمَ وَآلَ عِمْرَانَ عَلَى الْعَالَمِينَ

“Hakika Allaah Amemteua Aadam na Nuuh na kizazi cha Ibraahiym na kizazi cha ‘Imraan juu ya walimwengu.”

Akanambia: “kizazi cha Muhammad ilikuwepo pia hapo, lakini wakaiondosha na kuacha kizazi cha Ibraahiym na kizazi cha ´Imraan.”

Mhakiki ameelekeza katika “al-Bihaar”, “al-Burhaan”, “Ithbaat-ul-Hudaa”. al-´Ayyaashiy ametaja upokezi wa tatu wenye maana kama hiyo.

Baatwiniyyuun hawa wawili wamezidisha neno “kizazi cha Muhammd” katika Aayah hii halafu wanawazulia Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba wao ndio wameliondosha. Wamesapotiwa na mwandishi wa “al-Burhaan”, “as-Swaafiy”, “Ithbaat-ul-Hudaah” na Hishaam al-Mahlaatiy.

فَوَيْلٌ لَّهُم مِّمَّا كَتَبَتْ أَيْدِيهِمْ وَوَيْلٌ لَّهُم مِّمَّا يَكْسِبُونَ

“Basi ole wao kwa yale yaliyoandikwa na mikono yao na ole wao kwa yale wanayoyachuma.” (02:79)

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 36
  • Imechapishwa: 19/03/2017