06. Mashambulizi dhidi ya mfalme ´Abdul-´Aziyz ni mfano wa ugaidi

5- Mashambulizi ya kikandamizaji na ya kigaidi dhidi ya mfalme ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdir-Rahmaan al-Fayswal Aal Su´uud ni mfano mwingine wa ugaidi mbaya kabisa na wenye giza.

Asubuhi ya ijumaa mwaka 1353 alienda kutufu kwenye Ka´bah Twawaaf-ul-Ifaadhwah. Alikuwa amesindikizwa na mtoto wake mkubwa wa kiume Su´uud bin ´Abdul-´Aziyz wakiwa pamoja na kundi dogo la polisi na walinzi. Tahamaki mtenda dhambi mmoja aliyedanganywa akakitoa kisu chake mfukoni kutoka upande wa Shaam. Akalalamika maneno maovu na akamwendea mfalme. Polisi Ahmad bin Muusaa al-´Usayriy akajaribu kuingilia katikati, lakini yule aliyedanganywa akawahi kumdunga kisu na kumuua. Baada ya hapo yule mdanganyifu aliyepinda akamvamia askari mwingine na kumuua. Mwishowe mlinzi mmoja kutoka katika ulinzi wa kifalme akamshuti risasi na kumuua. Ndipo akajitokeza mtenda jinai mwingine ambaye na yeye akauawa na mlinzi mwingine. Wakati mhalifu wa tatu alipopata paniki na akajaribu kukimbia kutoka pale akapigwa risasi na polisi mmoja. Mfalme akaamrisha milango ya msikiti ifungwe ili aweze kukamilisha Twawaaf yake. Ajali hiyo ikajaribu kufunikwafunikwa ili mahuhaji wasiingiwe na khofu na wasiwasi. Lingeweza kuiathiri hajj yao.

Magaidi hawa watatu nyoyo zao zilikuwa zimejawa na machungu, chuki na hasadi dhidi ya kiongozi huyu ambaye Allaah ameihuisha Sunnah kupitia kwake. Mafunzo yake yaliinuka katika kisiwa cha Kiarabu na ulinganizi wa uongofu na nuru ilienea ulimwenguni wote wa Allaah. Allaah amrehemu na amwingize Peponi. Moto uwe kwa maadui wa dini ya Allaah ambao daima wanafanya bidii kueneza ufisadi juu ya ardhi ya Allaah.

 

  • Mhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Irhaab, uk. 14-15
  • Imechapishwa: 03/04/2017