06- Madhambi yanapelekea katika giza moyoni


Madhambi yanapelekea katika giza la kweli ambalo yule mtenda dhambi analihisi moyoni mwake. Analihisi kama anavyoona ule usiku wenye giza. Giza la maasi moyoni mwake linakuwa kama giza la usiku machoni mwake. Hakika utiifu ni nuru na maasi ni giza. Kadri ambavyo viza vitakuwa na nguvu zaidi ndivyo anavyozidi kudangana mpaka anatumbukia katika Bid´ah, upotevu na mambo mengine ya kuangamiza ilihali yeye si mwenye kuhisi hivo. Ni kama mfano wa kipofu anayetembea peke yake kwenye giza la usiku. Giza hili hupata nguvu zaidi mpaka likadhihiri machoni. Halafu hupata nguvu zaidi mpaka likaenea usoni na likawa jeusi mpaka kila mmoja akaliona.

  • Mhusika: Imaam Ibn Qayyim-il-Jawziyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ad-Daa’ wad-Dawaa’, uk. 66
  • Imechapishwa: 28/01/2018