06- Kushurutisha


10- Akipenda, ataunganisha pamoja na ile Talbiyah kushurutisha kwa ajili ya kuchelea chenye kuzuka njiani. Mfano wa vikwazo hivo inaweza kuwa maradhi au khofu. Aseme kama ilivyokuja katika mafunzo ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Ee Allaah! Kutoka kwangu kwenye Ihraam ni pale Utaponizuia.”

Akisema maneno hayo kisha akazuiliwa au ghafla akapatwa na maradhi, basi itafaa kujitoa katika Ihraam yake. Katika hali hii hatokuwa tena na uwajibu wa kuchinja au kuhiji mwaka unaofuata. Hata hivyo ikiwa ndio hajj yake ya kwanza, basi ni lazima kwake ailipe.

11- Hakuna swalah maalum kwa ajili ya Ihraam, lakini wakati wa swalah ukiingia kabla ya kuingia kwake Ihraam, na akaswali kisha akafanya Ihraam baada ya kuswali kwake, basi atakuwa na kiigizo kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), pindi alipoingia katika Ihraam baada ya swalah ya Dhuhr.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Manaasik-ul-Hajj wal-´Umrah, uk. 15
  • Imechapishwa: 06/07/2018