06. Kulenga kujionyesha katika mambo ya ki-´Ibaadah ni shirki ndogo

Miongoni mwa hayo ni yale yanayokuwa ndani ya moyo katika kujionyesha. Bi maana mtu akajionyesha kwa matendo. Mtu akafanya ´ibaadah uinje wake zikaonekana ni kwa ajili ya Allaah pamoja na kwamba anawaonyesha watu. Lengo anataka watu wamsifu, wamtape n.k. Huku ndio kujionyeasha. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Je, nisikwambieni kile ninachokukhofieni kuliko hata huyo al-Masiyh ad-Dajjaal?” Wakasema: “Ndio, ee Mtume wa Allaah!” Akasema: “Ni shirki iliyojificha.”

Shirki iliyojificha ni kujionyesha. Kwa sababu inakuwa ndani ya moyo na hakuna aijuaye isipokuwa Allaah pekee.

“Anasimama mtu kuswali na akaipamba swalah yake kwa kuwa anaona watu wanamwangalia.”[1]

Amesema (Ta´ala):

فَوَيْلٌ لِّلْمُصَلِّينَ الَّذِينَ هُمْ عَن صَلَاتِهِمْ سَاهُونَ الَّذِينَ هُمْ يُرَاءُونَ

“Basi adhabu kwa wanaoswali, ambao kuhusu swalah zao wanapuuza, ambao wanajionyesha.” (107:04-07)

Kujionyesha ni khatari. Ni jambo ambalo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kalikhofia juu ya Maswahabah zake. Kwa sababu kila mtu anapenda sifa, matapo, kuonekana kwa sura nzuri n.k., huenda hayo yakampelekea akaanza kujionyesha katika mambo ya ´ibaadah. Kujipamba mwili wake kwa mavazi na nguo nzuri, hili ni jambo linalotakikana kujipamba na kuvaa vizuri. Ama kuyapamba matendo yake mbele za watu ilihali hakusudii uso wa Allaah, bali kinyume chake anawakusudia watu, huu ndio msimba mkubwa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Kikubwa ninachokikhofia juu yenu ni shirki iliyojificha.” Wakasema: “Ni ipi hiyo, ee Mtume wa Allaah?” Akasema: “Ni kujionyesha.”

Imeitwa ´kujionyesha` (Riyaa`) kwa sababu malengo yake anataka watu wamuone.

[1] Ahmad (11270) na Ibn Maajah (4203). Nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh Sunan Ibn Maajah” (3389).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Aqiydah al-Islaamiyyah as-Swahiyhah https://www.youtube.com/watch?v=KqoTCYds6Cs&t=13s
  • Imechapishwa: 28/01/2019