Haifai kwa yeyote kufunga siku moja kabla na kwa hivyo akawa amefunga kabla ya kuyakinisha kuingia kwa mwezi mpya. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Msifunge kabla ya kuuona na msifungue kabla ya kuuona. Mkifunikwa na mawingu basi timizeni idadi ya siku thelathini.”

´Ammaar bin Yaasir (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Yule atakayefunga siku ya shaka basi kwa hakika amemuasi Abul-Qaasim (Swalla Allahu ´alayhi wa sallam).”

Kwa hiyo haijuzu kufunga ile siku ya tarehe 30 Sha´baan kwa nia kwamba iwe ndio siku ya kwanza ya Ramadhaan. Kuhusiana na yule ambaye ana mazowea ya kufunga na siku hiyo ikaangukia siku hiyo, wanachuoni wanasema kuwa hakuna neno. Hata hivyo anapaswa ajiepushe. Mtu anatakiwa kujiepusha na mambo yenye utata. Endapo atafunga siku hii kwa nia nyingine mbali na Ramadhaan na khaswa akiwa ni miongoni mwa wale ambao wanaigwa, kuna khatari wakamfuata wale wasiotambua.

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tafsiyr Aayaat-is-Swiyaam, uk. 11-12
  • Imechapishwa: 02/06/2017