06. Kisa cha Ibn Mas´uud na mwanamke aliyetegemea Qur-aan peke yake

Kwa mnasaba wa Aayah hii napendezwa na yale yaliyothibiti kwa Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´an) ambapo alijiwa na mwanamke na kumwambia: “Wewe ndiye unayesema: “Allaah amewalaani wenye kuwanyoa wenzao nyusi na wenye kunyolewa, wenye kuwachanja[1] wenzao… ?” Akajibu: “Ndio.” Mwanamke yule akasema: “Mimi nimesoma Kitabu cha Allaah chote kuanzia mwanzo mpaka mwisho na sijapata hicho unachokisema.” Akamwambia mwanamke yule: “Ikiwa kweli umefanya hivo basi umepata. Je, hivi hukusoma:

وَمَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانتَهُوا

“Kile alichokupeni Mtume, basi kichukueni, na kile anachokukatazeni, basi kiacheni.”?

Akajibu: “Ndio.” Ibn Mas´uud akamwambia: “Nimemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema: “Allaah amewalaani wenye kuwachanja wenzao… “

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

[1] Tattoo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Manzilat-us-Sunnah fiyl-Islaam, uk. 14-15
  • Imechapishwa: 10/02/2017