06. Kinga ya sita ya janga la corona: Du´aa kwa wingi

6- Kuomba du´aa kwa wingi

Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule ambaye katika nyinyi amefunguliwa mlango wa du´aa basi amefunguliwa milango ya rehema. Hakuna kitu ambacho Allaah aliombwa anachopenda kama kuombwa usalama.”

Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Du´aa inanufaisha kwa yenye kuteremka na ambayo hayakushuka. Hivyo basi, enyi wa Allaah, lazimianeni na du´aa!”[1]

[1] at-Tirmidhiy na wengineo.

  • Mhusika: Shaykh ´Abdur-Razzaaq bin ´Abdil-Muhsin al-´Abbaad
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Ashru Waswaayaa lil-Wiqaayah min-al-Wabaa’, uk. 10
  • Imechapishwa: 01/04/2020