06. Khatari ya mtu kutotendea kazi yale anayojifunza

Wema waliotangulia walikuwa wakiliogopa hili sana. Abu Dardaa´ (Radhiya Allaahu ´anh) alikuwa akisema:

“Kikubwa ninachochelea kwa Mola Wangu siku ya Qiyaamah ni pale ataponiita juu ya vichwa vya watu [na kunambia]: “Ee ´Uwaymir!” Niseme: “Nakuitikia Mola Wangu!” Aseme: “Ulifanya nini kwa kile ulichojifunza?”[1]

Vilevile Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekhabarisha kuwa: “Hautopiga tambo mguu wa mja siku ya Qiyaamah mpaka aulizwe kuhusu umri wake aliutumia katika nini, elimu yake aliifanya nini, mali yake aliipata na akaitumia vipi na mwili wake aliutumia katika nini?”[2]

Ee mwanafunzi! Hakika wewe utaulizwa siku ya Qiyaamah utapokuwa mbele ya Mola Wako pindi Allaah (´Azza wa Jall) atapowazungumzisha viumbe na kutakuwa hakuna baina Yake Yeye na wao mkalimani. Utaulizwa juu ya elimu yako uliifanyia nini. Ni lazima kwa aliye na elimu atende.

[1] Ibn-ul-Mubaarak katika “az-Zuhd war-Raqaaiq” (01/13-14), Ibn Abiy Shaybah katika “al-Muswannaf” (07/112/275) na wengineo

[2] at-Tirmidhiy (2714) ambaye amesema kuwa ni nzuri na Swahiyh. Ni Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh-ut-Targhiyb” (01/30)

  • Mhusika: Shaykh Sulaymaan bin Saliymillaah ar-Ruhayliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Ilm wa Wasaaailuh wa Thimaaruh
  • Imechapishwa: 22/10/2016