b) Ni haramu kwa mwanamke wa Kiislamu kuondosha nyusi au kuondosha baadhi yake kwa kutumia njia yoyote sawa ya kunyoa, kupunguza au kutumia nyenzo ya kuziondosha au kuondosha baadhi yake. Kwani kufanya hivi ndio Nams ambayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amemlaani mwenye kuifanya. Hakika amemlaani (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mwenye kuchonga nyusi zake na mwenye kuchongwa. Huyo ni yule mwanamke ambaye anaziondosha nyusi zake au, baadhi yake kwa madai eti ya kujipamba. Huku ni katika kubadilisha maumbile ya Allaah jambo ambalo shaytwaan aliliahidi kumwamrisha nalo mwanadamu, kama ambavo Allaah alisimulia juu yake:

وَلَآمُرَنَّهُمْ فَلَيُبَتِّكُنَّ آذَانَ الْأَنْعَامِ وَلَآمُرَنَّهُمْ فَلَيُغَيِّرُنَّ خَلْقَ اللَّـهِ

“Nitawaamrisha na hivyo watakata masikio ya wanyama na nitawaamrisha watabadili maumbile ya Allaah.”[1]

Imepokelewa katika “as-Swahiyh” kupitia kwa Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye amesema:

“Allaah amemlaani mwenye kufanya chanjo na mwenye kufanywa chanjo, mwenye kuchonga nyusi na mwenye kuchongwa nyusi na mwenye kufanya mwanya kwa ajili ya kutafuta urembo wanaoyabadilisha maumbile ya Allaah.”

Kisha akasema:

“Je, nisimlaani yule aliyelaaniwa na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndani ya Kitabu cha Allaah (´Azza wa Jall)?” akimaanisha maneno Yake:

وَمَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانتَهُوا

”Kile alichokupeni Mtume basi kichukueni na kile alichokukatazeni basi kiacheni.”

Hayo yametajwa na Ibn Kathiyr katika “Tafsiyr” yake[2].

Wanawake wengi wa leo wamepewa mtihani wa maradhi haya khatari ambayo ni dhambi kubwa miongoni mwa madhambi makubwa. Hali imefikia kiasi cha kwamba kuchonga nyusi imekuwa ni kama jambo la lazima miongoni mwa mambo ya lazima ya kileo. Wala haijuzu kwa mwanamke kumtii mume wake akimwamrisha kufanya hivo. Kwani ni maasi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tanbiyhaat, uk. 20-21
  • Imechapishwa: 22/10/2019