06. Hadiyth “Yule atakayeoga siku ya ijumaa… “


688- Abu Ayyuub al-Answaariy amesimulia ya kwamba amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

“Yule atakayeoga siku ya ijumaa, akajitia manukato ikiwa anayo, akavaa katika nguo zake nzuri kabisa, akatoka mpaka akafika msikitini, akaswali kiasi atachoweza, asimuudhi yeyote na akasikiliza mpaka akaswali, anakuwa ni mwenye kufutiwa [madhambi yake] mpaka ijumaa nyingine.”[1]

Ameipokea Ahmad, at-Twabaraaniy na Ibn Khuzaymah katika “as-Swahiyh” yake. Wapokezi wa Ahmad ni waaminifu zaidi.

[1] Swahiyh kupitia zengine.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/432)
  • Imechapishwa: 10/02/2017