42- Abu Ayyuub al-Answaariy amesimulia kutoka kw ´Awf bin Malik ambaye amesema:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alijitokeza kwetu akiwa ni mwenye kuogopa akasema: “Nitiini muda wa kuwa bado niko kati yenu. Jilazimieni na Kitabu cha Allaah na halalisheni halali zake na haramisheni haramu zake.”[1]

Ameipokea at-Twabaraaniy katika “al-Kabiyr”. Wapokezi wake ni waaminifu.

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/125)
  • Imechapishwa: 26/04/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy