06. Hadiyth “Mizozo juu ya Qur-aan ni ukafiri.”

143- Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mizozo juu ya Qur-aan ni ukafiri.”[1]

Ameipokea Abu Daawuud na Ibn Hibbaan katika “as-Swahiyh” yake.

144- at-Twabaraaniy na wengineo wameipokea kupitia kwa Zayd bin Thaabit (Radhiya Allaahu ´anh).[2]

[1] Nzuri kupitia zengine.

[2] Swahiyh. Kwa at-Twabaraaniy imekuja:

”Msizozane juu ya Qur-aan. Kwani hakika kuzozana juu yake ni ukafiri.” (4916)

Imesihi kwa ukamilifu huu kutoka kwa baadhi ya Maswahabah. Tazama ”as-Swahiyhah” (2419).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/170)
  • Imechapishwa: 07/05/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy