06. Hadiyth “Hudhurieni swalah ya ijumaa na sogeeni karibu na imamu… “


713- Samurah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hudhurieni swalah ya ijumaa na sogeeni karibu na imamu. Mtu atakuwa miongoni mwa watu wa Peponi halafu aje hali ya kuwa amechelewa ambapo acheleweshwe kutokamana na Pepo, ilihali ni miongoni mwa watu wake.”[1]

Ameipokea at-Twabaraaniy, as-Aswbahaaniy na wengineo[2].

[1] Nzuri kupitia zengine.

[2] Akiwemo Ahmad (05/10). Ilikuwa bora zaidi lau angerejesha kwake. Abu Daawuud amepokea mfano wake kwa mlolongo wa wapokezi mzuri, kama unaweza kupata katika ”Swahiyh Sunan Abiy Daawuud” (1015) na ”as-Swahiyhah” (365).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/445)
  • Imechapishwa: 25/01/2018