111- Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Hali itakuweje vipi kwenu pale mtapopatwa na fitina ambapo mdogo akawa mkubwa, mkubwa akawa mzee na ikachukuliwa kuwa ni Sunnah, siku moja itakapobadilishwa basi itachukuliwa ni kitu kisichojulikana?” Kukasemwa: “Ni lini wakati huo?” Akasema: “Ni pindi waaminifu wenu watakuwa wachache na viongozi wenu wakawa wengi, wanachuoni wenu wakawa wachache na wasomaji wenu wakawa wengi, kukasomwa kwa lengo jengine lisilokuwa dini na dunia ikafanyiwa bidii kwa matendo ya Aakhirah.”[1]

Ameipokea ´Abdur-Razzaaq kutoka kwa Ibn Mas´uud.

[1] Swahiyh kupitia zengine. Maneno hayo ni ya Swahabah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/155)
  • Imechapishwa: 03/05/2020
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy