721- ´Abdullaah bin ´Amr bin al-´Aasw (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaau ´alayhi wa sallam) amesema:

“Atakayeoga siku ya ijumaa, akajipaka manukato ya mke wake – kama atakuwa naye, akavaa nguo zake nzuri, asijipenyeze kati ya watu na asifanye upuuzi wakati wa mawaidha, basi madhambi yake yanafutwa mpaka ijumaa nyingine. Yule mwenye kufanya upuuzi na akajipenyeza kati ya watu basi anakuwa na Dhuhr.”[1]

Ameipokea Abu Daawuud na Ibn Khuzaymah katika “as-Swahiyh” yake kupitia kwa ´Amr bin Shu´ayb, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa ´Abdullaah bin ´Amr.

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/449)
  • Imechapishwa: 14/01/2018