181 – Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Anapotawadha mja muumini, au muislamu, ambapo akaosha uso wake, basi humwondoka usoni mwake kila dhambi aliyotazama kwa macho yake kwa yake maji, au kwa lile tone la mwisho la maji. Akiosha mikono yake,  basi humwondoka mikononi mwake kila dhambi aliyotenda kwa mikono yake kwa yale maji, au kwa lile tone la mwisho la maji. Akiosha miguu yake,  basi humwondoka miguuni mwake kila dhambi aliyotenda kwa miguu yake kwa yale maji, au kwa lile tone la mwisho la maji. Hatimaye anatoka hali ya kuwa amesafika na madhambi.”[1]

Ameipokea Maalik, Muslim na at-Tirmidhiy. Hata hivyo Maalik na at-Tirmidhiy hawakutaja miguu.

[1] Swahiyh.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Adhwiym bin ´Abdil-Qawiy al-Mundhiriy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb (1/189)
  • Imechapishwa: 14/04/2021
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy