06. Genge Lililojificha Nyuma Ya Mabomu Ya Misikiti


Utambue kuwa matendo machafu yanayofanywa na wapotevu ya kulipua na kuharibu kwa mabomu na kulipua magari na bali hata mabomu kwenye misahafu ya Qur-aan kwenye manyumba masafi ya Allaah wamechukua fikira na maelekezo hayo kutoka kwa Usaamah bin Laadin, Muhammad al-Mas´ariy, Sa´d al-Faqiyh, Abu Mus´ab az-Zarqaawiy na Ayman adh-Dhwaahiriy na warithi mfano wao, macho yenye kuwachunga na mikia yenye kuwaita majasiri na wapambanaji. Je, unajua kuwa kuna yeyote kabla ya watu hawa aliyewatangulia kufanya matendo machafu kama haya na ufisadi mkubwa kama kuua watu wasiokuwa na hatia, kuwatisha watu wenye amani na kuwachochea watu wengine dhidi ya wanachuoni wenye kutoa nasaha na watawala ili usalama wa nchi na maisha ya wananchi viweze kutikisika? Matokeo ya matendo hayo machafu yaliyotajwa ni kwamba kunapatikana madhara katika dini na dunia. Ni jambo linalojulikana na kila mtu.

  • Mhusika: ´Allaamah Zayd bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Waqafaat wa Ma´aalim, uk. 14
  • Imechapishwa: 14/12/2014