06. Du´aa wakati wa kumka usiku (kushtuka)


35- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kuamka usiku na akasema:

لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيكَ لَهُ لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ الْحَمْدُ لِلَّهِ وَسُبْحَانَ اللَّهِ وَلَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ وَاللَّهُ أَكْبَرُ وَلَا حَوْلَ وَلَا قُوَّةَ إِلَّا بِاللَّه العلىِّ العَظىم

“Hapana mola mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa Allaah, Mmoja asiyekuwa na mshirika. Ana ufalme na himdi na Yeye juu ya kila kitu ni Muweza. Himdi zote ni za Allaah. Ametakasika Allaah. Hapana mola mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa Allaah. Allaah ni Mkubwa. Hapana mabadiliko wala uwezo isipokuwa kwa msaada wa Allaah, Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika daima na Mwenye hekima wa yote daima.” Halafu akasema:

اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي

“Ee Allaah! Nisamehe” au akaomba Du´aa, huitikiwa. Akitawadha na kuswali basi Swalah yake hukubaliwa.”

36- Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Anayelala kitandani mwake hali ya kuwa ni mwenye Twahara na akamdhukuru Allaah (Ta´ala) mpaka pale anaposinzia hatojigeuza wakati hata mmoja usiku akimuomba Allaah kitu cha kheri duniani na Aakhirah isipokuwa Allaah Atampa nacho.”

37- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Wakati atapoamka mmoja wenu na aseme:

الحمد لله الذي عافاني في جسدي ورد علي روحي وأذن لي بذكره

“Himdi zote ni Zake Allaah ambaye Ameupa afya mwili wangu, Amenirudishia roho yangu na Kunifanya kumdhukuru.”

38- Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakati wa woga aliwafunza kusema:

أَعُوذُ بِكَلِمَاتِ اللهِ التَّامَّاتِ مِنْ غَضَبِهِ وَعِقَابِهِ وَمِنْ شَرِّ عِبَادِهِ وَمِنْ هَمَزَاتِ الشَّيَاطِينِ وَأَنْ يَحْضُرُونَ

“Najikinga kwa Maneno ya Allaah yaliyokamilika kutokana na Ghadhabu Zake, adhabu Zake na kutokana na shari za waja Wake na kutokana na upulizaji wa Shaytwaan na kila aliyekaribu kwa upande wake.”

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Swahiyh-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 39-41
  • Imechapishwa: 21/03/2017