06. Dalili ya tano kutoka katika Sunnah juu ya mikono ya Allaah

5- Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Kitu cha kwanza alichoumba Allaah (´Azza wa Jall) ni kalamu. Akaichukua kwa mkono Wake wa kulia – na mikono Yake yote ni ya kuume – na kuandika yote yatayotokea katika matendo mema na maovu, chenye unyevu na kikavu. Akakidhibiti Kwake kila kitu. Kama mnataka someni:

هَـٰذَا كِتَابُنَا يَنطِقُ عَلَيْكُم بِالْحَقِّ ۚ إِنَّا كُنَّا نَسْتَنسِخُ مَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ

“Kitabu Chetu hichi kinatamka juu yenu kwa haki; hakika Sisi tulikuwa tunaamrisha yaandikwe yale yote mlokuwa mkiyatenda.”

Ni kipi kitachoamrishwa kuandikwe kama sio kile ambacho tayari kimeshakwishapangwa?”[1]

Hadiyth ni nzuri. Nimefupisha mlolongo wa wapokezi ili mtu asije kuchoshwa nao.

[1] Ibn Abiy ´Aaswim (107) na ash-Shariy´ah, uk. 187, ya al-Aajurriy.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ithbaat-ul-Yad li-Laah Swifatan min Swifwaatih, uk. 17-18
  • Imechapishwa: 11/12/2018