06. Dalili ya nne kutoka katika Sunnah kwamba Allaah yuko juu ya viumbe

4- Abul-Mudhwaffar Ahmad bin Ahmad bin Muhammad bin Hamdiy ametukhabarisha: al-Qaadhwiy Abul-Husayn Muhammad bin Muhammad bin al-Husayn ametuhadithia: Abu Bakr Ahmad bin ´Aliy bin Thaabit al-Khatwiyb ametuhadithia: al-Qaasim bin Ja´far ametuhadithia: Abu ´Aliy al-Lu’lu-iy: Abu Daawuud as-Sijistaaniy ametuhadithia: Yaziyd bin Khaalid ar-Ramliy ametuhadithia: al-Layth bin Sa´d ametuhadithia, kutoka kwa Ziyaadah bin Muhammad, kutoka kwa Muhammad bin Ka´b al-Quradhwiy, kutoka kwa Fadhwaalah bin ´Ubayd, kutoka kwa Abud-Dardaa’ ambaye ameeleza kuwa amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

“Yule ambaye atahisi maumivu mmoja wenu, au akahisi maumivu ndugu yake, aseme: “Mola wetu ni Allaah ambaye yuko mbinguni. Limetakasika jina Lako.Amri Yako iko mbinguni na ardhini kama ambavyo huruma Yako iko mbinguni. Tusamehe madhambi na makosa yetu. Wewe ni Mola wa wazuri. Teremsha rehema Yako na dawa Yako kwa huyu anayehisi maumivu.” ili aweze kupona.”[1]

Ameipokea Abu Daawuud katika “as-Sunan”.

[1] Abu Daawuud (3892), Ahmad (6/21), ad-Daarimiy katika ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah”, uk. 18, al-Bayhaqiy katika ”al-Asmaa’ was-Swifaat”, uk. 533, na al-Laalakaa’iy katika ”Sharh Usuul I´tiqaad Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah” (648). Dhaifu kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Dhwa´iyf Sunan Abiy Daawuud” (3892).

  • Mhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ithbaatu Swifat-il-´Uluww, uk. 74-75
  • Imechapishwa: 26/02/2018