06. Baadhi ya alama za Ahl-ul-Bid´ah

Ahl-ul-Bid´ah wal-Ahwaa´ wana alama nyingi wanazotambulika kwazo:

1- Kuwatukana Ahl-ul-Athar. Abu Haatim ar-Raaziy (Rahimahu Allaah) amesema:

“Alama ya Ahl-ul-Bid´ah ni kuwatukana Ahl-ul-Athar.”[1]

2- Wana chuki kabisa kwa Ahl-ul-Hadiyth na wakati huo huo wanawanyamazia wapotevu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Wanawaua waislamu na wanawaacha washirikina.”[2]

Abu ´Uthmaan as-Swaabuuniy amesema:

“Alama ya Ahl-ul-Bid´ah iko wazi na dhahiri. Alama yao ya wazi ni chuki yao kubwa kwa wale wanaofikisha mapokezi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wanawadharau na kuwaita kuwa ni “Hashwiyyah”, “wajinga”, “Dhwaahiriyyah” na “Mushabbihah”. Wanaonelea kuwa mapokezi ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hayana elimu yoyote na elimu ni ile ambayo shaytwaan anawateremshia kupitia akili zao zilizooza, wasiwasi wenye giza ndani ya vifua vyao, nyoyo zao zisizokuwa na kheri yoyote na hoja zao zisizokuwa na matunda yoyote. Hao ndio ambao Allaah amewalaani.”[3]

3- Hutaka msaada kutoka mahakamani na kwa watawala kwa sababu hoja zao ni dhaifu. Huu ndio mfumo wao na uwezo wao wenye kukaribia kushindwa. Hujisaidiza kwa mahakama na watawala kwa kuwa ni sampuli ya shinikizo na woga.

4- Wana bidii yenye kupindukia katika ´ibaadah. Mzushi huongeza bidii yake katika ´ibaadah ili aweze kufikia uadhimisho, nafasi, mali na matamanio mengine ya kidunia. Ni jambo kubwa kuadhimishwa kwa ajili ya kujitenga na matamanio ya kidunia. Huoni jinsi watawa wanavyojitenga mbali na aina mbalimbali za starehe? Pamoja na hivyo wataingia Motoni. Allaah (Ta´ala) amesema:

وُجُوهٌ يَوْمَئِذٍ خَاشِعَةٌ عَامِلَةٌ نَّاصِبَةٌ تَصْلَىٰ نَارًا حَامِيَةً

“Nyuso siku hiyo zitadhalilika, zikifanya kazi ngumu na kuchoka, zitaingia na kuungua kwenye moto uwakao kweli kweli.” [4]

قُلْ هَلْ نُنَبِّئُكُم بِالْأَخْسَرِينَ أَعْمَالًا الَّذِينَ ضَلَّ سَعْيُهُمْ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَهُمْ يَحْسَبُونَ أَنَّهُمْ يُحْسِنُونَ صُنْعًا

”Sema: “Je, Tukujulisheni waliokhasirina mno kwa matendo? Ni wale ambao wamepoteza juhudi zao katika uhai wa dunia na huku wao wakidhani kuwa wanachuma mazuri [kwa yale wayafanyayo].”[5]

Kwa sababu ya matamanio yanayopatikana ndani yake wanaona kuwa kila wanachofanya ni rahisi. Pindi mtu wa Bid´ah anapoona kuwa fikira yake ni ya sawa huipenda. Ni kipi kitachomzuia ilihali anaona kuwa matendo yake ndio bora kuliko ya wengine wote na I´tiqaad zake ndizo zilizo salama kuliko za wengine wote?

كَذَٰلِكَ يُضِلُّ اللَّـهُ مَن يَشَاءُ وَيَهْدِي مَن يَشَاءُ

“Hivyo ndivyo Allaah anavyompotoa amtakaye na anamuongoa amtakaye.” [6]

Baadhi wanaweza kupewa mtihani wa Bid´ah pale wanapoona kuwa ni wenye kuipa nyongo dunia sana, wanyenyekevu, wenye kulia au mengine kwa sababu ya wingi wa ´ibaadah. Hata hivyo si hilo linaloteua ni kipi kilicho cha haki. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema kuwaambia Maswahabah wake juu ya Ahl-ul-Bid´ah:

“Mtazidharau swalah zenu kutokana na swalah zao, swawm zenu kutokana na swawm zao na kisomo chenu kutokana na kisomo chao.”[7]

[1] Sharh Usuul I´tiqaad Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah (1/179).

[2] al-Bukhaariy (3344) na Muslim (1064).

[3] ´Aqiydat-us-Salaf wa Aswhaab-il-Hadiyth, uk. 106.

[4] 88:02-04

[5] 18:103-104

[6] 77:31

[7] al-Bukhaariy (3610) na Muslim (1064).

  • Mhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Itmaam-ul-Minnah, uk. 77-79
  • Imechapishwa: 05/02/2017