06. at-Twartwuushiy kuhusu sherehe ya usiku wa nusu ya Sha´baan


Imaam Abu Bakr at-Twartwuushiy (Rahimahu Allaah) amesema katika kitabu chake “al-Hawaadith wal-Bid´ah” yafuatayo:

“Ibn Wadhdhwaah amepokea kutoka kwa Zayd bin Aslam ambaye amesema:

“Hatukuwakuta waalimu na wanazuoni wetu wakitilia umuhimu chochote kinachohusiana na nusu ya Sha´baan, Hadiyth ya Mak-huul wala hawakuona kuwa una fadhilah juu ya nyenginezo.”

Kulisemwa kuambiwa Ibn Abiy Mulaykah: “Hakika Ziyaad an-Numayr anasema kuwa ujira wa nusu ya Sha´baan ni kama ujira wa usiku wenye cheo.” Akasema: “Laiti ningelimsikia na mkononi mwangu ninayo fimbo basi ningempiga. Ziyaad msimulia visa.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tahdhiyr minal-Bid´ah, uk. 27
  • Imechapishwa: 17/01/2022