05. Wema wa Allaah kwa mwanadamu


… akamtoa nje kwa urafiki Wake na kumuwepesishia riziki Yake – Amemtoa nje kutoka tumboni mwa mama yake kwa urafiki Wake, upole na huruma Yake. Amempa wazazi wawili waliojaa mapenzi kipindi ambacho hawezi chochote; hamiliki juu ya nafsi yake manufaa wala madhara. Amesema (Ta´ala):

مَا أُرِيدُ مِنْهُم مِّن رِّزْقٍ وَمَا أُرِيدُ أَن يُطْعِمُونِ إِنَّ اللَّـهَ هُوَ الرَّزَّاقُ ذُو الْقُوَّةِ الْمَتِينُ

“Sitaki kutoka kwao riziki yoyote na wala Sitaki wanilishe. Hakika Allaah ndiye Mwingi wa kuruzuku, Mwenye nguvu madhubuti.”[1]

Akamfunza yale ambayo alikuwa hayajui na akampa fadhilah kubwa – Allaah (Ta´ala) amesemea:

الرَّحْمَـٰنُ عَلَّمَ الْقُرْآنَ خَلَقَ الْإِنسَانَ عَلَّمَهُ الْبَيَانَ

“Mwingi wa rehama. Amefundisha Qur-aan. Amemuumba mtu. Amemfunza ufasaha.”[2]

 Amemfunza mwanadamu yale asiyoyajua. Allaah amesema kumwambia Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

وَأَنزَلَ اللَّـهُ عَلَيْكَ الْكِتَابَ وَالْحِكْمَةَ وَعَلَّمَكَ مَا لَمْ تَكُن تَعْلَمُ ۚوَكَانَ فَضْلُ اللَّـهِ عَلَيْكَ عَظِيمًا

”Allaah amekuteremshia Kitabu na Hekima na akakufunza yale ambayo hukuwa unayajua – na fadhilah za Allaah juu yako ni kuu.”[3]

Allaah ndiye mwenye kumfunza mtu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akimshukuru Allaah na akisema katika du´aa zake:

“Sidhibiti kuweza kukusifu kama unavyostahiki. Wewe ni kama Ulivyojisifu Mwenyewe.”[4]

[1] 51:56-58

[2] 55:1-4

[3] 4:113

[4] Muslim (486).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Bayaan-ul-Ma´aaniy fiy Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy, uk. 13-14
  • Imechapishwa: 30/06/2021