05. Wapotevu wawili na mwongofu mmoja

Tunathibitisha kuwa Allaah ana nafsi isiyofanana na nafsi zengine. Amesema:

وَيُحَذِّرُكُمُ اللَّـهُ نَفْسَهُ

“Allaah anakutahadharisheni na nafsi Yake.”[1]

وَاصْطَنَعْتُكَ لِنَفْسِي

“Nimekuchagua kwa ajili Yangu.”[2]

Abu Hurayrah amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah (´Azza wa Jall) anasema: “Mimi ni vile anavyonidhania mja Wangu na mimi niko pamoja naye pindi anaponitaja. Akinitaja ndani ya nafsi yake, basi Namtaja ndani ya nafsi Yangu.”[3]

Tunathibitisha kwamba Allaah yuko juu ya ´Arshi Yake amelingana. Hivi ndivyo ilivyokuja katika Qur-aan katika Suurah saba: al-A´raaf, Yuunus, ar-Ra´d, Twaa Haa, al-Furqaan, as-Sajdah na al-Hadiyd.

Tunathibitisha kuwa:

“Mwingi wa huruma amemuumba Aadam kwa sura Yake.”

Ameipokea Ahmad bin Hanbal, Ibn Khuzaymah na wengineo. Vilevile imepokelewa:

“… kwa sura ya Mwingi wa huruma.”

Ameipokea ad-Daaraqutwniy, Abu Bakr an-Najjaad, Abu ´Abdillaah bin Battwah na wengineo.

Tunathibitisha kuwa Allaah ana vidole. Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Kuna mwanachuoni mmoja wa kiyahudi alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na akamwambia: “Ee Muhammad! Sisi tunakuta kuwa Allaah ataziweka mbingu juu ya kidole, ardhi juu ya kidole, miti juu ya kidole, maji juu ya kidole na viumbe vyengine vilivyobaki juu ya kidole. Halafu atasema: “Mimi ndiye Mfalme.” Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akacheka mpaka magego yake yakaonekana kwa kusadikisha maneno ya mwanachuoni huyu wa kiyahudi. Kisha akasoma maneno ya Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

وَمَا قَدَرُوا اللَّهَ حَقَّ قَدْرِهِ وَالْأَرْضُ جَمِيعًا قَبْضَتُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَالسَّماوَاتُ مَطْوِيَّاتٌ بِيَمِينِهِ

”Hawakumkadiria Allaah inavyostahiki kukadiriwa! Ardhi yote itakamatwa mkononi Mwake wa kuume siku ya Qiyaamah.”[4][5]

Ameipokea Hibatullaah at-Twabariy, al-Bukhaariy, Muslim na Abu ´Iysaa at-Tirmidhiy ambaye tamko yeye limekuja ifuatavyo:  Amenikhabarisha al-Mubaarak bin ´Abdil-Jabbaar as-Sayrafiy  kwenye kikao cha baba yangu (Rahimahu Allaah) kwenye msikiti wa Mansuur kwa cheni ya wapokezi wake kutoka kwa ´Abdullaah ambaye amesema:

”Kuna myahudi alikuja kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kusema: ”Ee Muhammad! Allaah ataziweka mbingu juu ya kidole, ardhi juu ya kidole na viumbe wengine juu ya kidole. Kisha atasema: ”Mimi ndiye Mfalme.” Ndipo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akaanza kucheka mpaka magego yake yakaonekana. Kisha akasoma:

وَمَا قَدَرُوا اللَّهَ حَقَّ قَدْرِهِ وَالْأَرْضُ جَمِيعًا قَبْضَتُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَالسَّماوَاتُ مَطْوِيَّاتٌ بِيَمِينِهِ

”Hawakumkadiria Allaah inavyostahiki kukadiriwa! Ardhi yote itakamatwa mkononi Mwake wa kuume siku ya Qiyaamah.”

Abu ´Iysaa amesema:

”Hadiyth hii ni nzuri na Swahiyh.”

Katika upokezi mwingine imekuja:

”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akacheka kwa kupendekezwa na kumsadikisha.”

Abu Sa´iyd amesimulia kwamba amemsikia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:

”Mola wetu atafunua muundi Wake ambapo atamsujudia kila muumini mwanaume na muumini mwanamke na watabaki [hali ya kusimama] wale ambao walikuwa wakisujudu duniani kwa kujionyesha na kutaka kusikika. Pale atapoenda ili kusujudu, tahamaki mgongo wake utarudi na kuwa talaka moja.”[6]

Anas ameeleza kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Allaah hufurahishwa na tawbah ya mja wake zaidi kuliko vile anavyofurahi mmoja wenu pale anapomkosa ngamia wake ambaye yuko na chakula na kinywaji chake juu yake. Kisha akamtafuta na asimpate. Baada ya hapo akalala chini ya mti na huku akisubiria kifo. Tahamaki ngamia yule amesimama juu yake. Akamshika khatamu na kwa furaha nyingi akasema: ”Ee Allaah! Wewe ni mja wangu na mimi ndiye Mola Wako.”[7]

´Abdullaah amesimulia kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimtaja ad-Dajjaal kisha akasema:

”Hakika ana chongo, lakini Mola wenu (´Azza wa Jall) hana chongo.”[8]

[7] Yule mwenye kuitakidi juu ya sifa hizi na mapokezi Swahiyh mfano wake kufanana inapokuja katika miili, aina, shakili na urefu, ni kafiri.

[8] Kuzikanusha sifa ni madhehebu ya Jahmiyyah. Yule mwenye kuzifasiri kutokana na lugha na majazi ni Jahmiy.

[9] Yule mwenye kuzipitisha kama zilivyokuja bila kuzipindisha maana, kuzifasiri, kuzifanya mwili wala kuzifananisha, kama walivyofanya Maswahabah na Taabi´uun, amefanya jambo la wajibu kwake.

[1] 03:28

[2] 20:41

[3] al-Bukhaariy (7405) na Muslim (2675).

[4] 39:67

[5] al-Bukhaariy (4811) na Muslim (2786).

[6] al-Bukhârî (4919) na Muslim (183).

[7] al-Bukhaariy (6308) na Muslim (2747).

[8] al-Bukhaariy (7131) na Muslim (2933).

  • Mhusika: Imaam Abul-Husayn Muhammad bin Abiy Ya´laa al-Hanbaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Kitaab-ul-I´tiqaad, uk. 26-31
  • Imechapishwa: 20/02/2019