05. Uwajibu wa Kiislamu wa kujua upotoshaji wa Raafidhwah

Katika hila za Raafidhwah ni kwamba chuki yao kubwa ya Qur-aan na Maswahabah imewafanya kupotosha Qur-aan na kuongeza na kupunguza ndani yake kutokana na matamanio yao yanayotoka kwenye chuki na madhehebu haribifu ya Baatwiniyyah.

Katika kitabu hichi utaona mambo mengi ya jarima hizi na khiyana ambazo mpaka hivi leo hazijatanguliwa kufanywa na yeyote.

Wanajifanya kulalamika juu ya kwamba Qur-aan imebadilishwa wakati wao wenyewe ndio wabadilishaji. Kisha isitoshe wanawatuhumu watu bora kabisa baada ya Mitume, bi maana Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ya kwamba wao ndio wamepotosha, kuongeza na kupunguza.

Uwajibu ulioko juu ya waislamu wote ni kuwa wanapaswa kutambua kuwa Raafidhwah Baatwniyyah wako wanabadilisha na kupotosha. Msomaji atajionea haya kwa macho yake. Kwa hakika sijaona yeyote anayejibebesha khatari hii na jarima kubwa. Wenye kufanya hayo wanatoka katika Uislamu na kuanguka mbali kabisa na Uislamu. Hali kadhalika hili pia linamgusa yule mwenye kuwa na imani kama hiyo na kupita katika njia yao wakati wanapowatuhumu Maswahabah ukafiri, upotoshaji wa Qur-aan na kuwa na chuki kwa watu wa familia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kwamba waliwapokonya uongozi na utawala.

Raafidhwah Baatwiniyyah wamepotosha na kuibadilisha Qur-aan sana kwa kutumia jina la kutaka kutetea haki juu ya watu wa familia ya Mtume ya uongozi na kwamba Maswahabah na Ummah waliwapokonya hilo na kuwadhulumu haki hiyo inayodaiwa, ´Aqiydah na Shari´ah yao inayozingatiwa kuwa ni muhimu kuliko haki ya Allaah na haki ya Manabii na Mitume.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intiswaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 33
  • Imechapishwa: 19/03/2017