Shaykh (Rahimahu Allaah) kama ilivyo kwa walinganizi wengine wote wenye kutengeneza alikutana na vizuizi na tuhuma za batili kutoka kwa wapinzani wake. Kulisemwa juu yake kwamba anatafuta ufalme na ukubwa. Haya yalisemwa pia kuhusu Mitume (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam):

مَا هَـٰذَا إِلَّا بَشَرٌ مِّثْلُكُمْ يُرِيدُ أَن يَتَفَضَّلَ عَلَيْكُمْ

“Huyu si chochote isipokuwa ni mtu kama nyinyi. Anataka ajifadhilishe juu yenu.”[1]

أَجِئْتَنَا لِتَلْفِتَنَا عَمَّا وَجَدْنَا عَلَيْهِ آبَاءَنَا وَتَكُونَ لَكُمَا الْكِبْرِيَاءُ فِي الْأَرْضِ

“Je, umetujia ili utugeuze kutokana na yale tuliyowakuta nayo baba zetu, na ili muwe na ukubwa na uadhama katika ardhi?”[2]

Kulisemwa juu yake kwamba ameleta madhehebu ya tano. Kwa ajili hiyo ndio maana wafuasi wake wakabandikwa jina la “Wahhaabiyyah”. Kwa sababu amelingania katika kitu kinachoenda kinyume na zile Bid´ah na shirki walizozowea. Uongo huu unakadhibishwa na Da´wah, vitabu na fatwa zake. Alibainisha kuwa anafuata ´Aqiydah ya Salaf na madhehebu ya Imaam Ahmad bin Hanbal. Hakupwekeka juu ya maoni yoyote yale. Ni vipi basi atakuwa na madhehebu maalum?

قُلْ هَاتُوا بُرْهَانَكُمْ إِن كُنتُمْ صَادِقِينَ

“Sema: “Leteni ushahidi wenu mkiwa ni wakweli.”[3]

Yule anayetaka kutambua utata aliorushiwa yeye na Da´wah yake basi arejee kusoma vitabu vyake na yale aliyoyajibu juu ya shubuha hizo. Haki iko wazi kabisa kama lilivyo wazi jua na haikufunikwa na uongo na ubabaishaji. Kwa hivyo mtu asitegemee maneno ya wale wapinzani wake juu yake yeye na juu ya Da´wah yake.

[1] 23:24

[2] 10:78

[3] 02:111

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: I´aanat-ul-Mustafiyd bi Sharh Kitaab-it-Tawhiyd, uk. 13
  • Imechapishwa: 22/07/2019